• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

Maendeleo na Ustawi wa Jamii


UTANGULIZI

Idara ya maendeleo na ustawi wa Jamii ina vitengo sita ambavyo kwa pamoja vinatekeleza majukumu yafuatayo:


SHUGHULI ZA MAENDELEO

•Kuhamasisha Jamii kushiriki katika kazi za maendeleo ya sekta ya mbalimbali ikiwa ni sekta ya Kilimo Mifugo, Afya, Elimu na Maji

•kuwezesha Jamii kushiriki katika hatua ya kupanga, kuibua na kusimamia miradi kupitia mikutano na vikao ngazi ya mitaa, na kata.


UKIMWI

Katika jiji la Arusha hali halisi ya maambukizi ya VVU/ Ukimwi yanaonyesha kupungua kutoka asilimia 3.1 hadi 2.2 Idara inaendelea kutekeleza shughuli zifuatazo katika kudhibiti maambukizi ya VVU kama ifuatavyo:

•Kutoa mafunzo ya kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kwa vikundi, Vicoba na Sacoos  ili familia kujiwekea akiba.

•Kuhamasisha WAVIU (watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi)kujiunga kwenye vikundi, Saccos, na Vicoba kwa wanawake kwa ajili ya kujiongezea kipato ngazi ya familia.

•Kutoa msaada kwa watoto yatima waliotambuliwa ngazi ya Kata na mtaa husika Katika masuala ya Elimu kwa kuwalipia ada, na sare.

•Kutoa  kielimu katika masuala ya ujasiriamali kwa vikundi, Saccos na Vicoba vya WAVIU (watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi)

•Kutoa ushauri nasaha na upimaji wa afya kwa hiari kwa Jamii ili kujua afya zao.



UTAFITI NA MIPANGO

•Kutoa ushauri wa kitaalamu katika masuala ya uanzishaji na uendeshaji wa NGOS, CBOs, na FBOS zinazoto huduma kwa Jamii kwa ujumla

•Kutoa elimu kwa Jamii juu ya ushirikishwaji katika hatua ya kupanga, kuibua, kutekeleza, kufuatilia na kufanya tathimini ya miradi ya kilimo na ufugaji

•Kutoa ushauri na elimu ya ujasiriamali kwa Jamii katika masuala ya utunzaji wa kumbukumbu, huduma kwa wateja



WANAWAKE, JINSIA NA WATOTO


Kuwezesha wanawake kiuchumi,

•Kuwezesha Jamii kuunda na kusajili vikundi, Saccos na Vicoba kwa wanawake ili kuweza kukopesheka na taasisi za kifedha pamoja na halmashauri kupitia mfuko wa maendeleo ya wanawake hatimaye kurahisisha Urejeshaji wa Mikopo hiyo.



•Kusimamia haki za watoto ngazi ya familia kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya mwaka 2009

•Kusimamia na kutetea haki za wanawake kwa kuzingatia dhana ushirikishwaji wa wanawake katika ngazi za  maamuzi.


MAENDELEO YA VIJANA

Kuwezesha vijana kiuchumi

•Kuwezesha na kutoa elimu ya uundaji na usajili wa vikundi na Saccos kwa vijana ili kuweza kukopesheka na tasisi za kifedha pamoja na halmashauri kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana na hatimaye kurahisisha Urejeshaji wa Mikopo hiyo.

•kutoa ushauri wa kitaalamu kwa vijana katika masuala ya afya ya msingi, stadi za kazi, malezi na makuzi  


 MFUKO WA AFYA YA JAMII-TIBA KWA KADI (TIKA)

 Ni mpango wa hiari unaoiwezesha jamii kupata huduma za matibabu kwa mwaka  mzima kwa kuchangia mara moja tu kiasi cha fedha kwa kadiri jamii yenyewe katika Halmashauri husika itakavyoamua. Katika Jiji la Arusha kiasi cha uchangiaji ni Tsh. 12,000 kwa kaya yenye Baba , mama na wategemezi wanne waliochini ya miaka 18, mtu mmoja moja, wanafunzi sita katika kundi moja. Mpango huu unalenga wakulima na wafugaji,wavuvi,wajasiriamali,vikundi vya uzalishalishaji mali na tasisi.

Aidha Idara ya Maendeleo ya jamii inaendelea na kuratibu na kuhamasisha jamii kujiunga na mpango wa Tiba Kwa Kadi (TIKA) kwa ajili ya kupata huduma ya Afya kwa gharama nafuu na kutoa maelekezo ya vituo vya kutolea huduma ya Afya

MPANGO WA LISHE

•Kuhamasisha jamii kuhusiana na umuhimu wa lishe bora sambamba na umuhimu wa upimaji wa afya mara kwa mara ili kujua hali zao za afya hasa lishe.

•Kuhamasisha Jamii na kusimamia uanzishaji wa bustani za nyumbani kwa ajili ya kuboresha lishe ya familia.


MAJUKUMU YA  USTAWI WA JAMII

(i)HUDUMA KWA FAMILIA, WATOTO NA MALEZI YA AWALI YA MTOTO

Kitengo hiki kinatoa huduma zake kwa kuzingatia Sera, Miongozo, Kanuni na sheria zifuatazo:

•Sheria ya Ndoa Na. 5 ya mwaka 1971;

•Sheria ya mtoto ya mwaka 2009;

•Sheria ya kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu ‘’The Anti-Trafficking in Persons’’ Act, 2008

Huduma zinazotolewa ni pamoja na:-

Huduma za usuluhishi wa ndoa zenye mifarakano;

Huduma ya matunzo kwa watoto walio kwenye ndoa zenye mfarakano;

Huduma ya matunzo kwa watoto wanaozaliwa nje ya ndoa;

Huduma ya makao ya kulelea watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi;

Huduma ya  malezi ya kambo na kuasili

Huduma ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya  watoto wadogo.

Huduma ya Malezi, Matunzo na Ulinzi shirikishi Jamii kwa watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi (community based care, support and protection of orphans and vulnerable children

Huduma kwa familia zenye dhiki

(ii) MAREKEBISHO YA TABIA NA HAKI ZA MTOTO KISHERIA:

Kitengo hiki kinatoa huduma  kwa kuzingatia Sera, Miongozo, Kanuni na     Sheria mbalimbali. Sheria hizo ni;

•Sheria ya mtoto ya mwaka 2009

•Sheria ya Huduma za Majaribio na Ujenzi wa Tabia (Sura Na.247)

•Sheria ya Makosa ya Kujamiiana Na.4 ya Mwaka 1998

•Sheria ya Kanuni za adhabu (Sura ya 16)

•Sheria ya Huduma kwa jamii Na.6 ya Mwaka 2002


Huduma zinazotolewa ni pamoja na:-

Haki za watoto/vijana (Juvenile Justice

Huduma katika Mahabusi za watoto

Huduma za shule ya maadilisho

Huduma kwa watoto watukutu (Juvenile delinquents)

Huduma zitolewazo katika Mahakama ya watoto

Huduma kwa watoto wanaoishi mitaani

Huduma ya elimu juu ya athari ya pombe na madawa ya kulevya


(ii) HUDUMA KWA WATU WENYE ULEMAVU NA WAZEE:

Kitengo hiki kinatoa huduma  kwa kuzingatia Sera, Miongozo, Kanuni na     Sheria zifuatazo:

Sera:

•Sera ya Taifa ya Wazee (2003);

•Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu (2004).

Sheria:

•Sheria ya Watu Wenye Ulemavu (Na. 9, ya 2010)


Huduma zinazotolewa ni pamoja na:-

Mafunzo ya Stadi za kazi kwa watumishi wa Ulemavu:

Utengemao kwa Watu wenye Ulemavu:

Marekebisho

Matunzo kwa Watu wenye Ulemavu/Wasiojiweza:

Huduma ya Utengemao kwa wazee walio katika makazi:

Huduma za ushauri kwa Wazee:

Nyenzo za Kujimudu:

Huduma kwa Vyama/Asasi za Watu wenye Ulemavu:


(ii) PROGRAMU ZINAZOSIMAMIWA NA IDARA YA USTAWI WA JAMII


Mpango shirikishi jamii wa malezi, matunzo na ulinzi kwa yatima na watoto walio katika mazingira hatarishi

Mpango wa Uwezeshaji Haki Jamii

Programu ya stadi za malezi ya watoto walio katika mazingira hatarishi

Programu ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto wadogo 0-8

Mpango wa Uzuiaji Usafirishaji Haramu wa Watu


















Matangazo

  • KUSITISHWA KWA TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA BONDENI CITY December 06, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI March 14, 2023
  • TANGAZO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KUHUSU KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA MAOMBI YA MIKOPO YA HALMASHAURI July 14, 2022
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA August 11, 2022
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YATIA FORA UGAWAJI WA MIKOPO, YAMWAGA ZAIDI YA BILIONI 2 ZA MIKOPO KWA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU.

    March 22, 2023
  • JIJI LA ARUSHA LATIA FORA UGAWAJI WA MIKOPO, LAMWAGA ZAIDI YA BILIONI 2 ZA MIKOPO KWA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU.

    March 22, 2023
  • JIJI LA ARUSHA LATIA FORA UGAWAJI WA MIKOPO, LAMWAGA ZAIDI YA BILIONI 2 ZA MIKOPO KWA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU.

    March 22, 2023
  • ZIARA YA KAMATI YA SIASA MKOA WA ARUSHA KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHAA

    March 21, 2023
  • Tazama zote

Video

ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa