• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

Elerai

TAARIFA YA  KATA YA ELERAI 

UTANGULIZI:

Kata ya Elerai ni miongoni mwa kata 25 zinazounda Jiji la Arusha.  Kata hii ina kaya 6052 na wakazi wa kata hii ni 28,813.

UTAWALA:

Kata hii ina watumishi 13 nao ni;

Afisa Afya

Afisa maendeleo ya jamii

Mratibu wa Elimu

Afisa mifugo

Watendaji wa mitaa 6

Walinzi 2

Afisa mtendaji wa kata.

ULINZI NA USALAMA.

Hali ya ulinzi na usalama ni nzuri kwa kipindi chote cha miezi mitatu (3) hakuna tukio lolote la uhalifu lililotokea katika kata. Ulinzi unaotumika katika kata ni wananchi kujilinda wenyewe kwa kuweka zamu.

KUITISHA VIKAO VYA MITAA:

Kwa kipindi cha mwezi May – Julai vimefanyika vikao 39 na kukamilisha muhtasari 39.

MAENDELEO YA KATA YA ELERAI.

Kata ya Elerai inatoa pongezi kubwa kwa maendeleo ya Kata yaliyofanyika hususani kama ifuatavyo:

Ujenzi wa paa la pili la soko lenye thamani ya Tsh.100,000,000/=

Ujenzi wa Zahanati umekamilika

Ujenzi wa madarasa manne ya Sekondari ya Elerai yenye

Ukarabati wa madarasa matatu ya shule ya sekondari elerai yenye thamani ya Tsh.1,3000,000/=

USAFI WA MAZINGIRA:

Hali ya usafi wa mazingira inaridhisha kwani wananchi wamehamasika kufanya usafi wa maeneo yao yote yanayowazunguka.

Elimu ya usafi inaendelea kuimarika kulingana na siku tunazofanya usafi ya Jumamosi ya kwanza ya mwezi na ya mwisho wa mwezi kila mwezi.

USAFI WA SOKO LA ELERAI:

 Kwa ushirikiano wa watendaji wa mitaa pamoja na wafanyabiashara wa soko tunafanya usafi ndani na nje ya soko pamoja na vyoo vya soko.

USAFI WA BARABARA YA MAJENGO NA MITARO

Usafi huu ulifanyika vizuri kushirikiana na wafanyabiashara walioko maeneo hayo kando kando ya bara bara na ndani ya mitaro.

UKAGUZI WA MAZINGIRA WA MAMA LISHE.

Wafanyabiashara wa mama lishe wamekaguliwa na kupewa elimu kuhusu kuvaa uniform (sare za kazi) wanapokuwa kwenye biashara zao, maji ya wateja ya kunawia mikono yawe moto kulipia shilingi elfu tano (5000) na kupima afya zao, kusafisha maeneo wanayofanyia biashara na kuahakikisha yawe masafi siku zote.

TAARIFA YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII

 

0.1 SHUGHULI ZILIZOFANYIKA.

1.1 KUFUATILIA MAREJESHO YA MIKOPO KWA VIJANA NA WANAWAKE.

Kwa kata ya Elerai vikundi viatatu (3) vya wadaiwa sugu, kikundi kimoja kipo mtaa wa Samanga kinaitwa Maisha Plus na viwili majengo A ambavyo ni Tukundane na Tarajio W. Group.  Ufuatao ni mchanganuo katika Jedwali.

JINA LA KIKUNDI

MWAKA

MKOPO

MKOPO + RIBA

REJESHO

SALIO

TARAJIO W. GROUP
2014
2,000,000/=
2,200,000/=
1,824,000/=
376,000/=
TUKUNDANE
2014
1,500,000/=
1,165,000/=
1,030,000/=
620,000/=
MAISHA PLUS
2010
1,000,000/=
1,100,000/=
550,000/=
550,000/=
JUMLA

4,500,000/=
4,950,000/=
3,404,000/=
1,546,000/=

Kwa Kata ya Elerai kikundi cha Vijana wadaiwa sugu ni kimoja tu.  Kipo Mtaa wa Remtula.

JINA LA KIKUNDI

MWAKA

MKOPO

MKOPO + RIBA

REJESHO

SALIO

GLOFAHABEEL
2014
1,500,000/=
1,650,000/=
1,462,500/=
187,500/=
JUMLA

1,500,000/=
1,650,000/=
1,462,500/=
187,500/=

1.2  USIMAMIZI UJAZAJI WA MIKATABA

Niliweza kusimamia ujazaji Mkataba kikoba cha UMJ kilichopitishwa na WDC kitakachotumika kupitishia Mikopo ya vikundi vingine, pia niliwakutanisha na viongozi wa vikundi vilivyoomba mkopo mwaka 2016 kwa majina ni B. Mabaju, Sindeni, Usia na Neema Limca.

KUKUTANA NA VIKUNDI NA KUTOA USHAURI/ MAELEKEZO.

Kukutana na vikundi na kutoa ushauri kuhusu usajili wa vikundi, pia kutoa ushauri mambo ya kiuchumi kama vile kila Mwanakikundi awe na shughuli ya kumpatia kipato.  Na wote kwa pamoja wawe na malengo ili wanaposema wanavunja mzunguko wapeane mrejesho walichofanikiwa na sio kukiri kwa kugawana faida tu.

NA.

JINA LA KIKOBA

MTAA KILIPO


HAPA KAZI TU
SHAMSI

NIWEZESHE
SHAMSI

FUTURE
MAJENGO B

WAWAEL
MAJENGO B

ALFA
MAJENGO A

UKOMBOZI
BURKA

1.4. KUSIMAMIA UHAWILISHAJI FEDHA KWA KAYA MASKINI.

 Mpango huu unaendeshwa na TASAF awamu ya tatu, nimekuwa nikishiriki awamu zote mbili kwa malipo ya miezi miwili miwili, kwa awamu zote mbili huwa nashiriki katika mitaa 04 kwa muda wa siku nne.  Tarehe 23 – 26/5/2016 nishiriki mitaa ifuatayo RC kata ya Mushono, Jamhuri kata ya daraja mbili, Olmatejo B kata ya Sakina, Majengo kata ya Levolosi.  Tarehe 1/8/2016 – 4/8/206 nilishiriki Mitaa ya mita 200 Ngarenaro, Daraja mbili, Sokoni 1 na Olorieni.

1.5:  KUANDAA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.

Kusimamia maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika tarehe 16/6/2016 shule ya msingi Burka.  Walitoa ujumbe kuhusu haki za watoto kwa njia ya nyimbo, shairi, ngonjera. Watoto walitoa msisitizo kwa jamii kushiriki kuwalinda na vitendo vya kikatili.

1.6:  KUWASILISHA/ KUHAKIKI MAJINA KAMILI YA WATOTO WALIOOMBA KUPEWA MAHITAJI YA SHULE.

Majina kumi (10) tu ndio walioomba kupatiwa mahitaji ya shule na ndio yalipitishwa na WDC na kuwasilisha majina hayo ofisi ya maendeleo ya jamii depot.

1.7: UCHAGUZI WA KAMATI YA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI YA KATA.

Kamati hii ilichaguliwa kwa kufuata muundo, walipatiwa mafunzo tarehe 15/7/2016 shule ya msingi Meru, ili kushirikiana na kamati za mitaa kutoa huduma kwa watoto hao.

1.8: UCHAGUZI KUHUSU TIBA KWA KADI (TIKA)

Elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi kwenye mikutano ya mitaa na vikundi vya jamii juu ya umuhimu wa kujiunga na tika.

2.  MIKOPO

Vikundi vya wadaiwa sugu wamepewa ilani ya miezi mitatu (3) wawe wamemaliza kurejesha mkopo wa kikundi.  Wenyeviti wa mitaa vikundi vilipo wamepewa nakala ya ilani kwa usimamizi na Mh. Diwani kwa ufuatiliaji, hivyo nahitaji ushirikiano

Wanakikundi ambao hawajulikani walipohamia tushirikiane na wenyeviti wa mitaa husika na wanakikundi waliobaki ili kujua walipohamia.

TAARIFA YA UTEKELEZAJI – IDARA YA ELIMU TAREHE 9.8.2016.

UTANGULIZI:

Shule zilizopo katika kata ambazo zina usajili ni kama ifuatavyo:

SERIKALI:

Elerai msingi, Azimio s/msingi, Burka s/msingi na Elerai sekondari.

BINAFSI:

Arusha Modern, Arusha Intergrated, Majengo, St. Thadeus, Joseph zote hizi ni za msingi na Sekondari ya Bishop Kisula.

IDADI:

Shule za serikali zina idadi ya wanafunzi na madawati kama ifuatavyo:

JINA LA SHULE

IDADI YA WANAFUNZI

MADAWATI

WAV
WAS
JML
HITAJIKA
YALIYOPO
PUNGUFU
BURKA

580

607

1187

392

423

-

AZIMIO

393

413

806

280

289

-

ELERAI S/MSINGI

862

884

1746

581

591

-

ELERAI SEK

643

710

1353

1353

1353

-

MIUNDO MBINU:

JINA LA SHULE

MATUNDU YA VYOO

VYUMBA VYA MADARASA

HITAJIKA
ILIYOPO
PUNGUFU
HITAJIKA
VILIVYOPO
PUNGUFU
BURKA
WAV: 23
         53
WAS: 3O
24
29

27

23

4

AZIMIO
WAV: 16
          37
WAS: 21
10
27

19

11

8

ELERAI S/MSINGI
WAV: 34
          78
WAS: 44
8
70

39

17

22

ELERAI SEK
WAV: 25
          60
WAS: 35
20
40

30

23

7


UWIANO:         MATUNDU YA VYOO

VYUMBA VYA MADARASA


WAV:  1: 25
WAS: 1: 20

1: 45

MAFANIKIO:

Shule zote zina madawati ya kutosh na hakuna upungufu.

Kukamilika kwa vyumba vinne vya madarasa Elerai Sekondari, pamoja ukarabati wa vyumba vitatu vya madarasa.

Kukarabatiwa kwa vyoo matundu 8 shule ya msingi Elerai na viko katika hali nzuri.

Mfadhili AVCO ameanza kujenga vyumba viwili S/M Elerai vipo hatua ya msingi. Pia kufunika shimo kubwa la choo.

Hali ya taaluma mashuleni ni nzuri.  Hii ni kutokana na matokeo ya majaribio mbali mbali yanayofanyika.

Fedha za elimu msingi zimeendelea kutumwa shuleni, kutoka Januari – Machi zimepokelewa kama ifuatavyo:-

ELERAI

BURKA

AZIMIO

ELERAI SEKONDARI

5,555,000/=
4,261,000/=
3,461,000/=
Fidia ya ada: 16,261,000/=
Capitation: 15,364,000

CHANGAMOTO:

Mapungufu ya matundu ya vyoo kama ilivyo kwenye jedwali.  Ni pamoja na vyumba vya madarasa na miundo mbinu ya kupekeka maji kwenye vyoo vinavyotumiwa na wavulana Elerai Sekondari.

Tatizo la nyumba za walimu Shule ya msingi Burka zilizopo ndani ya eneo la Elerai sekondari.

Nyumba ya Mwl. iliyopo Elerai Sekondari ambayo inahitaji kukamilishwa.

Kukosekana kwa uzio wa shule kwa shule zote za msingi.

Kutokuwepo kwa majengo ya utawala kwa shule ya Azimio, Elerai s/msingi, Elerai Sekondari na kusababisha kubadili chumba cha darasa kuwa ofisi.

Kukosekana kwa stoo hasa kwa shule ya Elerai s/msingi na Azimio s/msingi.

Baadhi ya wazazi kutokuona umuhimu wa uchangiaji chakula shuleni japo elimu inaendelea kutolewa.

MIFUGO:

IDADI YA MIFUGO NA KAYA:

KAYA ZINAZOFUGA
NG’OMBE
MBUZI
KONDOO
MBWA WAFUGWAO
KUKU
BATA
74
185
105
25
10
1162
78

LISHE KWA MIFUGO:

Hali ya malisho na maji ni ya kuridhisha.

MIUNDO MBINU YA MIFUGO

Hakuna miundo ya mifugo

MAGONJWA

Magonjwa yaliyojitokeza katika kata ya Elerai ni:

NA
UGONJWA
AINA YA MIFUGO
PATWA
TIBIWA
KUFA
PONA
DAWA ILIYOTUMIKA

NDIGANA BARIDI
Ng’ombe
5
5
-
5
O.T.C 10%
Multivitamin

HOMA YA KIWELE
Ng’ombe
2
2
-
2
Peniallon

NAGANA/NDOROBO
Ng’ombe
1
1
-
1
Novidium
O.T.C 10%

MINYOO
Ng’ombe
Mbuzi
3
19
3
19
-
3
19
Albendazole 10%

CHANJO KWA MIFUGO:

Hakuna chanjo yoyote kwa mifugo iliyotolewa.

HUDUMA NYINGINEZO (HUSBANDRY PRACTICES).

AINA YA MIFUGO

IDADI

HATUA

NJIA ILIYOTUMIKA

USHAURI

MBUZI
2
Kukata pembe
Msumeno
Kurekebisha mifugo
NG’OMBE
1
kuhasi
Burdizo
Kuboresha mifugo

MBWA WAZURURAJI:

Mbwa wapatao 48 wameuwawa katika mtaa wa Kware na zoezi hili ni endelevu.

CHANGAMOTO NA MAFANIKIO

8:1:  CHANGAMOTO:

Gharama za pembejeo za kilimo na mifugo kuwa juu.

Wafugaji wengi hufuga kwa mazoea/uzoefu.

8:2:  MAFANIKIO:

Wafugaji wapatao watano (5) kunufaika na Elimu juu ya ufugaji bora na wenye tija.

MIRADI ILIYOIBULIWA.

ELIMU:

Kupatiwa jengo la Utawala kwa shule ya Elerai sekondari, Azimio s/msingi na Elerai s/msingi.

Kunahitajika matundu ya vyoo kama ifuatavyo:

i)  Elerai s/msingi     -        matundu 70

ii)  Azimio s/msingi   matundu 27

iii) Burka s/msingi    -        matundu 29

iv) Elerai Sek   -        matundu 40

Vyumba vya madarasa.

i)  Elerai s/msingi     -        vyumba 22

ii)  Azimio s/msingi   vyumba 08

iii) Burka s/msingi    -        vyumba 04

iv) Elerai Sek   -        vyumba 07

HUDUMA ZA JAMII

i)  Barabara inayotoka kibaoni hadi TANAPA ipitishwe greda na kuweka vifusi

ii)  Barabara ya mwisho wa hiace (stendi) ipanuliwe kwani ajali zimekuwa nyingi na gari kubwa inapita kwa tabu.

iii) Barabara ya kutoka TANAPA hadi Arusha meat itengenezwe kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa magari makubwa.

iv)  Ofisi ya Kata ya Elerai igeuzwe kuwa sehemu ya kulaza wagonjwa na jengo lililopembeni ya ofisi ya kata ili kuwa ofisi ya kata /likarabatiwe..

v)  Eneo la mgodini liandaliwe kwa ajili ya soko la mahindi ili lisikae bila faida.

vi) Barabara ya Tarimo mtaa wa Burka ifunguliwe upya na kujazwa vifusi inayoungana na Sakina.

vii)  Matengenezo ya barabara ya kuansia kanisani hadi mabanzini kwa kuwekea vifusi.

viii) Kuwekwa mitaro ya maji kwa bara bara ya shamsi kibanda maziwa.

ix)  Eneo la stendi majengo juu kupatikane vyoo vya kulipia.

x) Uhitaji wa viwanja vya michezo (kuna eneo linalouzwa mtaa wa URUNDINI na linafaa kugeuzwa kuwa kiwanja cha michezo).

xi)  Mkandarasi wa taka, taka zimemzidi.

xii)  Kukamilisha ujenzi wa jengo la utawala/madarasa ya Elerai sekondari.

Matangazo

  • KUSITISHWA KWA TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA BONDENI CITY December 06, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI March 14, 2023
  • TANGAZO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU KUHUSU KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA MAOMBI YA MIKOPO YA HALMASHAURI July 14, 2022
  • TANGAZO LA UUZAJI WA VIWANJA August 11, 2022
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA YATIA FORA UGAWAJI WA MIKOPO, YAMWAGA ZAIDI YA BILIONI 2 ZA MIKOPO KWA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU.

    March 22, 2023
  • JIJI LA ARUSHA LATIA FORA UGAWAJI WA MIKOPO, LAMWAGA ZAIDI YA BILIONI 2 ZA MIKOPO KWA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU.

    March 22, 2023
  • JIJI LA ARUSHA LATIA FORA UGAWAJI WA MIKOPO, LAMWAGA ZAIDI YA BILIONI 2 ZA MIKOPO KWA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU.

    March 22, 2023
  • ZIARA YA KAMATI YA SIASA MKOA WA ARUSHA KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHAA

    March 21, 2023
  • Tazama zote

Video

ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa