• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Arusha City Council
Arusha City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Arusha

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Fedha na biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Primary Education
      • Elimu Sekondari
      • Usafishaji na Mazingira
      • Works and Infrastucture
      • Water
      • Mipango, Uchumi na takwimu
      • Mipango miji
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
    • Vitengo
      • Sheria
      • Tekinolojia ya habari Mawasiliano na Mahusiano
      • Manunuzi
      • Internal Audit
      • Uchaguzi
      • Ufugaji wa nyuki
    • Kata
      • Baraa
      • Daraja II
      • Elerai
      • Engutoto
      • Kaloleni
      • Kati
      • Kimandolu
      • Lemara
      • Levolosi
      • Moivaro
      • Moshono
      • Murriet
      • Ngarenaro
      • Olasiti
      • Olmoti
      • Oloirien
      • Osunyai
      • Sakina
      • Sekei
      • Sinon
      • Sokon I
      • Sombetini
      • Terrat
      • Themi
      • Unga Ltd
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Usafi wa Mazingira
    • Elimu
    • Biashara
    • Maendeleo ya Jamii
    • Leseni
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Wabunge na Madiwani
    • Kamati za kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maadili
      • Kudhibiti UKIMWI
    • Ratiba
      • Ratiba za Vikao
      • Ratiba ya kumuona Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • STUDY ONLINE
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Hotuba
    • Taarifa kwa umma

VITAMBULISHO KWA WAFANYABIASHARA WADOGO JIJINI ARUSHA ALMAARUFU KAMA MACHINGA KUANZA KUTOLEWA TAREHE 19 MWEZI HUU

Posted on: December 17th, 2018

Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Jiji la Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo wakati wa kikao chake na wafanyabiashara hao mapema leo hii katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Katika kikao hicho Mhe. Gambo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imejikita katika kutatua changamoto za wananchi hasa wanyonge hivyo katika harakati za kumkomboa mwananchi katika lindi la umasikini na hatimaye uchumi wa kati serikali imetengeneza  vitambulisho maalum  kwa ajili ya  kuwatambua  rasmi wafanyabiashara wadogo almaarufu kama machinga kote nchini.

Mhe. Gambo alisitiza kuwa vitambulisho hivyo ni mahsusi kwa watu wasio katika sekta rasmi  wakiwemo machinga hivyo  serikali haitamvumilia mfanyabiahara yoyote mwenye eneo la kufanyia biashara kutaka kuvuruga utaratibu na kuwakosesha haki wanaostahili.

“Kama lilivyo agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  vitambulisho hivyo vinawalenga wafanyabiashara ambao mzunguko wao wa mauzo ni chini ya shilingi milioni 4  kwa mwaka  hivyo kigezo  cha mfanyabiashara husika kupatiwa kitambuliso ni utanzania wake na si chama chake cha siasa wala dini yake”. Alisema Mhe. Gambo

“Lengo la vitambulisho hivyo si kuwatambua watu wasio katika sekta rasmi pekee bali ni pamoja na kutatua changamoto ya migogoro na migongano ya kimaslahi baina ya wwafanyabiashara wasiokuwa na maeneo rasmi na wale wenye maeneo rasmi ya kufanyia biashara zao”. Aliongeza Mhe. Gambo.  

 

 

Kabla ya kuanza kikaohicho  Mhe. Mrisho Gambo alitoa fursa kwa wafanyabiashara wote  pamoja na uongozi wao kuainisha changamoto zao pamoja na mapendekezo yao  juu ya kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanyia biashara ambapo Mwenyekiti wa Machinga Jiji la Arusha Bi. Amina Njoka alisema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo kama machinga ni kuhusu wafanyabiashara wenye maeneo rasmi ikiwemo madukani na masokoni  kukimbia sehemu zao na kujifananisha na machinga hali inayopelekea kuonekana machinga wote ni wavunjifu wa taratibu na kanuni za nchi.

Naye mmoja wa machinga wa soko la NMC Samunge  Bw. Philipo Kwaiamesema kuwa wangependa serikali ya Mkoa na Halmashauri ya Jiji iwapatie maeneo rasmi ya kufanyia biashara zao na hatua  za kisheria zichukuliwe dhidi ya wafanyabiashara wa eneo la mataa ya friends corner kwani hupanga biashara zao katika eneo la barabara hivyo kusababisha adha kwa watumiaji wa barabara pamoja na kuhatarisha usalama wao wenyewe. 

Katika kujibu maoni na kero za wafanyabiashara hao Mhe. Gambo alisema kuwa baada ya zoezi la kutoa vitambulisho hivyo  uongozi wa Jiji na Mkoa utapita katika masoko yote kukagua sehemu zilizoachwa wazi na watakabidhiwa wasiokuwa na maeneo.

Zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho hivyo litafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzi Tehehe 19-21  Disemba mwaka huu katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi Ya  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini pamoja na Ofisi ya  Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.

MWISHO.

Matangazo

  • NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA KUSAFIRI NJE YA NCHI KWA WATUMISHI WA SERIKALI January 16, 2025
  • MATOKEO YA USAILI WA MCHUJO KADA YA MTENDAJI WA MTAA NA KADA YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU October 06, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO LA MIKOPO October 29, 2024
  • Tazama zote

Habari za hivi punde

  • JIJI LA ARUSHA LAZINDUA MITAMBO MIPYA

    January 28, 2025
  • MKURUGENZI KAYOMBO AKABIDHIWA OFISI

    August 21, 2024
  • WANAWAKE NA WASICHANA KUJENGEWA UWEZO WA KISHIRIKI NAFASI ZA UONGOZI

    August 20, 2024
  • NENDENI MKAONGEZE UFANISI

    August 19, 2024
  • Tazama zote

Video

JIUNGE NA MFUMO WA TAUSI
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • MIRADI ILIYOKAMILIKA
  • MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA
  • SISI NI NANI
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira safi Maisha bora

Viunganishi Linganifu

  • TAMISEMI
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Tovuti ya ajira
  • Tovuti ya Ikulu
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Location Map

Wasiliana nasi

    20 Boma Street 23101

    Sanduku la Posta: 3013

    Simu: 0272548072

    Simu ya Mkononi: 0272545768

    Barua Pepe: cd@arushacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha .Haki zote Zimehifadhiwa